Hawa Ndio Wachezaji Waliotoka Vinara kwenye Tuzo za BALLON D'OR

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

1 year ago
rickmedia: hawa-ndio-wachezaji-waliotoka-vinara-kwenye-tuzo-ballon-dor-185-rickmedia

Lionel Messi ameshinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mara ya (8), mara nyingi kuliko Binadamu yoyote aliyewahi kucheza mchezo wa Soka, Tuzo hizo amezishinda mwaka 2009, 2010, 2011, 2012, 2015, 2019, 2021 na 2023. Akiwa na umri wa miaka (36) na siku (128), Lionel Messi amekuwa mchezaji wa pili mwenye umri mkubwa zaidi kwenye historia kutwaa tuzo ya Ballon d'Or baada ya Sir Stanley Matthews aliyetwaa Ballon d'Or akiwa na umri mkubwa kuliko Messi (41 yrs) mwaka (1956).Messi amekuwachezaji wa kwanza kwenye historia kutwaa Ballon d'Or akiwa anacheza soka nje ya Ulaya.


Jude Bellingham (20) ameshinda tuzo ya mchezaji bora kijana U21 wa Dunia Kopa Trophy kwenye tuzo za Ballon d'or 2023 akiwashinda 


◉ Jamal Musial

◉ Pedri

◉ Eduardo Camavinga

◉ Gavi

◉ Xavi Simons

◉ Alejandro Baldé

◉ António Silva

◉ Rasmus Højlund


Vinicius Jnr ameshinda tuzo ya Utu na Ubinadamu, Socrates Award kwenye tuzo za Ballon d'or kutokana na kupambana na Ubaguzi wa rangi michezoni na kujitoa kusaidia watu wasiojiweza.


Erling Haaland ameshinda tuzo ya mshambuliaji bora wa Dunia wa mwaka 'Gerd Muller Award' kwenye tuzo za Ballon d'or.


◉ Games — 53

◉ Goals scored — 52


Golikipa wa Argentina, Emiliano Martinez ameshinda tuzo ya Golikipa bora wa Dunia 'THE 2023 YACHINE TROPHY' kwenye tuzo za Ballon d'or 2023


Klabu ya Manchester city imechaguliwa kuwa klabu bora ya mwaka Duniani 2023.


Imeandikwa Sostenes