Kituo cha 'NBA Africa' kilichopo chini ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu wa Marekani (NBA), kimefungua rasmi Ofisi yake katika mji wa Westlands, Nairobi
Kituo hicho cha kukuza Vipaji katika Mchezo wa Kikapu kitaunga mkono mipango yote ya biashara na maendeleo ya mpira wa Kikapu ya Ligi za Kenya.
Ofisi ya Nairobi inakuwa ya 5 kufunguliwa Barani Afrika baada ya Cairo (Misri), Dakar (Senegal), Johannesburg (Afrika Kusini) na Lagos (Nigeria)
Mkurugenzi Mtendaji wa NBA Africa, Victor Williams amesema hatua hiyo itaruhusu kufanya kazi kwa karibu zaidi na Wadau ili kukuza Mchezo huo kwa Mashabiki na Wachezaji wa Kenya.