Azikwa akiwa hai siku 7 ili kurekodi maudhui ya Youtube mubashara

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: azikwa-akiwa-hai-siku-ili-kurekodi-maudhui-youtube-mubashara-735-rickmedia

Mwandaa maudhui wa mtandao wa Youtube, James Stephen Donaldson maarufu kama ‘Mr Beast’ ameshangaza watu wengi duniani kwa kuandaa tukio la mazishi yake angali akiwa hai na kukaa kaburini kwa muda wa siku saba huku akiwa anajirekodi na kuwasiliana na watu walio nje.

Mr Beast mwenye umri wa miaka 25 alitengeneza jeneza lenye mfumo wa umeme ambalo pia lina mfumo wa hewa, camera, chakula na maji.

Hata hivyo, katika siku saba ambazo Mr Beast ‘alizikwa hai’ aliendelea kuwasiliana na rafiki zake ambao waliweka kambi juu ya kaburi lake huku wakifuatilia usalama na afya yake.

Tukio hilo lilirushwa mubashara katika ukurasa wake wa Youtube ambao una wafuasi milioni 212 na video hiyo akiwa kaburini imefikisha jumla ya watazamaji milioni 63 ikiwa ni siku mbili tu zipite tangu akiwa ameiachia rasmi.