Akiri Hatia Ya Makosa Nane ya Kigaidi

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

5 hours ago
rickmedia: akiri-hatia-makosa-nane-kigaidi-241-rickmedia

Mfanyabiashara wa vitu vya Sanaa mwenye asili ya Nigeria na Uingereza, #OchukoOjiri, amekiri mashtaka manane yanayohusiana na kufadhili ugaidi baada ya kushutumiwa kuuza kazi za sanaa kwa mwanaume anayeshukiwa kutoa fedha kwa kundi la Hezbollah.

Ochuko Ojiri mwenye umri wa miaka 53, ambaye ameonekana kwenye vipindi maarufu vya BBC kwa miaka kadhaa, alihudhuria Mahakama ya Westminster Magistrates leo asubuhi. Alishtakiwa kwa kosa maalum chini ya kifungu cha 21a cha Sheria ya Ugaidi ya mwaka 2000.

Hili linajumuisha makosa manane ya kushindwa kutoa taarifa wakati wa shughuli za kibiashara katika sekta iliyo chini ya usimamizi wa kisheria, ambayo sasa amekiri kuyafanya.

Mashtaka dhidi ya mtu huyo maarufu wa televisheni, ambaye jina lake kamili ni Oghenochuko Ojiri, yanahusiana na kipindi cha kati ya Oktoba 2020 hadi Desemba 2021.

Uchunguzi uliopelekea kufunguliwa kwa mashtaka dhidi ya Ojiri ulifanywa na maafisa kutoka Kitengo cha Kitaifa cha Upelelezi wa Fedha za Kigaidi, ambacho ni sehemu ya Kikosi cha Kukabiliana na Ugaidi cha Polisi wa Metropolitan.

Ojiri, kutoka magharibi mwa London, hapo awali alikuwa mmiliki wa duka la mitindo ya zamani katika mji mkuu lililoitwa Pelicans & Parrots ambalo lilifungwa mnamo Oktoba 2021.