Mwanamitindo #SanRechalGandhi amefariki dunia baada ya kuripotiwa kutumia kupita kiasi dawa za usingizi. Tukio hilo limetokea mjini Puducherry, na limeibua majonzi makubwa katika tasnia ya mitindo na urembo Nchini India.
#SanRechalGandhi alikuwa akijulikana si tu kwa mafanikio yake katika jukwaa la urembo, bali pia kwa msimamo wake thabiti dhidi ya ubaguzi wa rangi (colourism) na juhudi zake za kutetea usalama wa wanawake. Alikuwa miongoni mwa wanawake wachache waliotumia majukwaa ya kimataifa kuzungumzia masuala ya kijamii yanayowakumba wanawake wa Asia Kusini.
Marehemu aliwakilisha India katika matukio kadhaa ya kimataifa ya mitindo na aliheshimiwa kwa sauti yake ya kipekee katika harakati za kijamii.
Polisi bado wanaendelea kuchunguza mazingira ya kifo chake.