Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.
Kupitia mitandao yake ya kijamii Rais Samia ameandika, "Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natuma salamu zetu za rambirambi kwa Mheshimiwa, Bola Ahmed Tinubu, Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria, familia ya Rais Buhari na wananchi wa Nigeria,"
Buhari, aliyekuwa rais kabla ya aliyepo sasa, aliripotiwa kusafiri kwenda Uingereza mwezi Aprili kwa uchunguzi wa kawaida wa afya, lakini baadaye hali yake ilizorota na akaugua.
Enzi za uhai wake, Muhammadu Buhari alitawala Nigeria kuanzia mwaka 2015-2023.