Morgan Hertage Wamtambulisha Msanii Mpya.

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

13 hours ago
rickmedia: morgan-hertage-wamtambulisha-msanii-mpya-822-rickmedia

Bendi maarufu ya muziki wa reggae , #MorganHeritage, imemtambulisha rasmi #JamereMorgan kama mwimbaji mpya wa kundi hilo baada ya kifo cha #PeetahMorgan.

#JamereMorgan, ambaye ni mtoto wa #GrampsMorgan, alifanya onyesho lake la kwanza rasmi kama mwimbaji kiongozi wa #MorganHeritage kwenye tamasha la kihisia la Summerjam Festival nchini Ujerumani, ambalo pia lilikuwa onesho la kwanza kubwa la kundi hilo tangu kifo cha #Peetah mnamo Februari 2024.

Mpaka sasa, familia ya #Morgan haijatoa taarifa rasmi kuhusu chanzo halisi cha kifo cha #Peetah, huku #GrampsMorgan, katika mahojiano ya hivi karibuni na vyombo vya habari, akieleza tu kwamba: “Ilikuwa ni ugonjwa wa nadra sana ambao hakuna aliyetarajia.”

#MorganHeritage ni mojawapo ya bendi zinazotambuliwa sana duniani katika muziki wa reggae. Ilianzishwa mwaka 1994 na watoto watano wa msanii maarufu kutoka Jamaica, #DenroyMorgan.

Watoto hao #PeetahMorgan (ambaye sasa ni marehemu), #GrampsMorgan, #UnaMorgan, #LukesMorgan, na #MrMojo walikulia Marekani lakini walilea mizizi yao katika muziki wa Jamaica na utamaduni wa Rastafari.

Kwa miaka mingi, kundi hili la kifamilia limefanya maonesho mbalimbali duniani kote na kutoa album nyingi, huku wakijihusisha kikamilifu katika uandishi na utayarishaji wa nyimbo zao wenyewe.

Mwaka 2016, Morgan Heritage walishinda Tuzo ya Grammy kupitia album yao Strictly Roots, iliyotwaa tuzo ya Best Reggae Album.