Siku chache kabla ya maonyesho makubwa ya #Beyoncé jijini Atlanta, tukio kubwa la wizi limeripotiwa. Watu wasiojulikana wamevamia magari ya Dancer wake na choreographer wa #Beyoncé na kuiba hard drive zenye taarifa nyeti.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, vifaa hivyo vilivyoporwa vilikuwa na nyimbo ambazo bado hazijatoka rasmi, video za nyuma ya pazia (behind-the-scenes), pamoja na mipango ya maonyesho yajayo ya #Beyoncé.
Tukio hilo linadaiwa kutokea karibu na eneo la mazoezi ya maonyesho. Mamlaka za usalama zimeanza uchunguzi rasmi ili kuwabaini wahusika na kurejesha vifaa vilivyoibiwa.
Hadi sasa, #Beyoncé wala timu yake hawajatoa tamko rasmi kuhusu tukio hilo, lakini mashabiki wengi wameonyesha wasiwasi juu ya uwezekano wa nyenzo hizo kuvuja mitandaoni na kuathiri maandalizi ya onyesho.