50 Cent akataa BILIONI 8 kutumbuiza kwenye Kampeni za Trump

-rickmedia: Rick

Rick

10 months ago
rickmedia: cent-akataa-bilioni-kutumbuiza-kwenye-kampeni-trump-403-rickmedia

Rapa 50 Cent anadai kukataa Dau la Zaidi ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 8 ili kutumbuiza kwenye moja ya Mikutano ya Kampeni za Mgombea Urais wa Marekani Donald Trump

Akizungumza kwenye kipindi cha Breakfast Club cha nchini Marekani 50 Cent amesema kuwa anaogopa sana kujihusisha na Siasa pamoja na mambo ya dini kwani yanaleta mgawanyiko kwa watu na machafuko

"Ni kweli nilipokea ofa ya kutumbuiza kwenye Mkutano wa kampeni wa Trump kwenye ukumbi wa Madson Square Garden lakini nilikataa. Unajua naogopa sana siasa, ukijiingiza kwenye siasa lazima kuna wakukupinga waibuke, sio wote watakubaliana na wewe. Naepuka siasa na Dini, Dini ndiyo ilimgombanisha Kanye West na baadhi ya mashabiki zake. Kiufupi mimi Sipendi siasa", amefunguka 50 Cent