Msanii wa Muziki wa Hiphop #ChidiBenz amefunguka maoni yake kuhusu muziki wa sasa ulivyo huku akisema kuwa Wasanii wa sasa wanachokitaka ni kuwa Mastaa,Waingize pesa,Wavae na kuishi vizuri na wapate wanawake wazuri lakini hawajui wanachokifanya.
Mbali na hivyo #Chidi amegusia wimbo wa #Nitongoze wa #Rayvanny na #DiamondPlatnumz na kusema Wimbo kama huo watoto wataimbaje huku akisisitiza kuwa hana tatizo na Msani.
"Nawapenda wasanii wote na wanamuziki wote na wadogo zangu wote lakini 'Nitongoze' mtoto wangu anaimbaje? Anamtoto yule anaitwa Latifah kama mtoto wangu wa kwanza lakini mtoto wake ile anaiimbaje? Na nisieleweke tofauti sina tatizo nae"- #ChidiBenz akiwa kwenye kipindi cha ##Shajara #CloudsTv
Mbali na hivyo #ChidiBenz amefunguka na kusema kuwa licha ya kuwa na Wimbo na Msanii namba 1 Tanzania lakini bado watu wanamwambia hawamsikii kitu ambacho hakielewi.
"Watu wengi nakutana nao wananiambia hatukusikii nawauliza mnanisikiliza? Mimi nina wimbo mpya na Diamond baba, iweje hunisikii? Super star wenu namba 1 nina wimbo nae halafu mnasema hamnisikii?"