Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu raia wa Burundi, Ferdnand Ndikuriyo (27) maarufu 'Chuma cha Chuma', kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh500,000 baada ya kupatikana na hatia ya kuwepo nchini Tanzania bila kuwa na kibali.
Chuma cha Chuma ambaye ni msanii wa muziki na mkazi wa Mbezi Louis, anadaiwa kutenda kosa lake, Septemba 18, 2024 eneo la Las Vegas Casino, Upanga wilayani Ilala.
Uamuzi huo umetolewa leo, Jumatano Februari 5, 2025 na Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa huyo.
Hakimu Ruboroga amesema mshtakiwa ni mkosaji wa mara ya pili na kwamba anahitaji kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine.