Rais Donald Trump aigeukia Afrika Kusini kuinyima misaada?

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: rais-donald-trump-aigeukia-afrika-kusini-kuinyima-misaada-653-rickmedia

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema bila kutaja ushahidi, kwamba "tabaka fulani za watu" nchini Afrika Kusini walikuwa wakitendewa ‘vibaya sana’ na kwamba atakata ufadhili wa nchi hiyo hadi suala hilo litakapochunguzwa.

Trump amebainisha hilo jana, Februari 2, 2025 katika mtandao wake wa Truth akisema kuwa baadhi ya wananchi amekuwa wakifanyiwa ukatili.

"Afrika Kusini inanyakua ardhi, na inawatendea watu wa tabaka fulani vibaya sana," amesema Trump na kuongeza;

"Marekani haitasimama kwa hilo, tutachukua hatua. Pia, nitakata ufadhili wote ujao kwa Afrika Kusini hadi uchunguzi kamili wa hali hii utakapokamilika!" amesema.

Haijulikani ni nini kilisababisha hadi Trump kuchapisha ujumbe huo na hata ulipotafutwa Ubalozi wa Afrika Kusini mjini Washington DC haukujibu chochote kuhusu hilo.