Rais Samia Aguswa na Kifo cha Sheikh Muhammad Iddi

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

5 days ago
rickmedia: rais-samia-aguswa-kifo-cha-sheikh-muhammad-iddi-523-rickmedia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani ametoa pole kufuatia kifo Cha Sheikh Muhammad Iddi (Abuu Iddi), Imamu Mkuu wa Msikiti wa Mwinyiamani, Mshauri wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, kilichotokea leo januari 30,2025 Jijini Dar es Salaam.

Rais Samia Ametoa Salamu za pole kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, ambapo ameeleza namna alivyopokea taarifa ya kifo hicho Kwa masikitiko..

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Sheikh Muhammad Iddi (Abuu Iddi), Imamu Mkuu wa Msikiti wa Mwinyiamani, Mshauri wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Ali Mbwana na Mratibu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, kilichotokea leo Alhamisi, Januari 30, 2025.

Natoa salamu za pole kwa familia, Mufti Mkuu wa Tanzania, Waislamu wote nchini, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.

Tumeondokewa na mtu aliyeipenda nchi yake, mwalimu katika imani, mlezi wa wengi katika imani, mpenda haki, mpenda ukweli, umoja, amani na utulivu wa nchi yetu, aliyetumia muda wake mwingi kuyasimamia na kufundisha hayo kupitia mawaidha yake.

Mwenyezi Mungu ampe Kauli Thabit, amsamehe makosa yake, amzidishie katika mizani mema aliyotenda, na ampe nafasi katika Pepo yake.