Brian Mundubile,mikononi mwa polisi kwa tuhuma za Uhaini

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 hour ago
rickmedia: brian-mundubilemikononi-mwa-polisi-kwa-tuhuma-uhaini-957-rickmedia

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Zambia (NRPUP), Brian Mundubile, amekamatwa na kuzuiliwa na mamlaka kwa tuhuma za uhaini, baada ya kuingia mafichoni kufuatia kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti 13.

Matokeo hayo rasmi yalionyesha kuwa Rais aliyepo madarakani, Hakainde Hichilema, alishinda kwa asilimia 60 ya kura dhidi ya asilimia 38 alizopata Mundubile.

Siku moja baada ya uchaguzi huo, kikosi cha usalama kilivamia eneo linalohusishwa na kiongozi huyo jijini Lusaka, ambapo waziri wa zamani aliuawa na wanasiasa kadhaa kukamatwa.