Kocha Pep Guardiola amefunguka kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake na Cristina Serra katika filamu mpya ya makala ya Manchester City. Akizungumza na wachezaji wake, Pep alisema: “Nimetalikiana na mwanamke mrembo zaidi duniani—mke wangu, au mke wangu wa zamani.
"Ninampenda sana kiasi kisichoelezeka, lakini tulikosa ule mwamko na shauku ya mapenzi. Je, ninampenda? Ndiyo, bila shaka. Yeye ananipenda? Ndiyo, lakini tulikosa ule mwamko na shauku.”
Kisha akatumia fursa hiyo kuwaambia wachezaji wake: “Katika maisha yenu, chochote mtakachofanya, kifanyeni kwa shauku na moyo wote. Sitaki wachezaji wazuri tu; nataka wachezaji wenye shauku.”