Marekani yaweka vikwazo dhidi ya mashirika ya ndege ya Iran

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 hour ago
rickmedia: marekani-yaweka-vikwazo-dhidi-mashirika-ndege-iran-847-rickmedia

Marekani imeweka vikwazo dhidi ya mashirika 27 ya ndege ya Iran pamoja na kampuni na watu wengine 36 wanaohusishwa na sekta ya usafiri wa anga ya nchi hiyo.

Hazina ya Marekani imesema walengwa hao wanadaiwa kusaidia kusafirisha silaha, wanajeshi na mizigo haramu, huku baadhi yao wakihusishwa na Mahan Air.

Waziri wa Hazina wa Marekani, Scott Bessent, amesema hatua hiyo inalenga kuongeza shinikizo la kiuchumi dhidi ya Tehran, huku kampuni au watu wanaofanya biashara na mashirika hayo wakitakiwa kuwa tayari kwa hatua zaidi za kifedha.

Vikwazo hivyo pia vinawalenga kampuni katika UAE, Uturuki, Malaysia na Kazakhstan zinazotoa huduma kwa sekta hiyo ya anga.