TANZIA: Mume wa Rais Samia afariki Dunia leo hii

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 hour ago
rickmedia: tanzia-mume-rais-samia-afariki-dunia-leo-hii-972-rickmedia

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi ametangaza taarifa ya msiba wa Hafidh Ameir Hassan, Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza leo, Septemba 7, 2026, Makamu wa Rais amesema “kwa masikitiko makubwa, nawajulisha taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Hafidh Ameir Hassan, Mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kilichotokea leo tarehe saba Septemba 2026, majira ya saa mbili ya asubuhi, katika Hospitali ya Emilio Mzena Zanzibar, alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo,”

“Ninatoa pole kwa Mheshimiwa Rais, familia, ndugu, jamaa na marafiki, na Watanzania wote kwa msiba huu, mpango wa mazishi unaendelea kufanyika Kizimkazi, Zanzibar,”