Tukio la kushtusha na lenye kuzua gumzo kubwa mitandaoni limetokea baada ya mwanamke mmoja raia wa Marekani, Kiera Williams, kukiri kupitia mtandao wa Facebook kuwa alimvua wigi kichwani dada yake aliyekuwa marehemu katikati ya shughuli ya mazishi.

Kiera alieleza kuwa kabla ya kifo cha dada yake, wawili hao walikuwa hawazungumzi kabisa kutokana usaliti ambapo marehemu alikuwa akitembea na mzazi mwenzake (baby daddy) kwa siri.
"Ndio, nilichukua wiku yangu kutoka kwa dada yangu kwenye mazishi yake na wala sijali! Pamoja na familia nzima kukasirika, mimi sijali kabisa!" aliandika Kiera kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Mwanamke huyo ameongeza kuwa hana mpango wa kumsamehe dada yake hata kama amefariki, na wala hayuko tayari "kuwa mtu mwenye busara" au kuachilia suala hilo. Post hiyo imezua mjadala mzito mtandaoni huku wengi wakishtushwa na kitendo hicho cha kuvunja heshima ya msiba.