Rigathi Gachagua akata Rufaa kuondolewa madarakani

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 days ago
rickmedia: rigathi-gachagua-akata-rufaa-kuondolewa-madarakani-888-rickmedia

Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, amekata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu uliothibitisha kuondolewa kwake madarakani, akipinga uamuzi kwamba hatua hiyo haiwezi kubatilishwa licha ya ukiukwaji wa baadhi ya haki zake za kikatiba.

Gachagua anadai Mahakama Kuu ilikosea kisheria kwa kusema uamuzi wa Seneti wa kumwondoa madarakani ulikuwa wa mwisho na hauwezi kupitiwa na mahakama, wakati mahakama hiyo ilibaini kuwa baadhi ya taratibu za kumwondoa zilikiuka haki yake ya kusikilizwa.