Barron Trump ni mtoto wa mwisho mwenye umri wa miaka 20 wa Rais Donald Trump na Melania Trump, anakadiriwa kuwa na utajiri wa takriban dola milioni 150, kiasi kinachozidi kile cha mama yake Mzazi.
Takwimu hiyo, inayotokana na makadirio ya jarida la Forbes yaliyonukuliwa na Yahoo Finance na vyanzo vingine, inatokana hasa na nafasi yake kama mmoja wa watu wa awali kuunga mkono sarafu za kidijitali (crypto) na kama mwanzilishi mwenza wa mradi wa familia wa World Liberty Financial (WLFI) uliozinduliwa mwishoni mwa mwaka 2024.
Alipata takriban dola milioni 80 kutokana na mauzo ya 'tokeni' na anamiliki sehemu kubwa ya tokeni za WLFI zilizofungwa (pamoja na umiliki katika bidhaa zinazohusiana nazo kama vile sarafu thabiti ya USD1);
Umiliki huu unawakilisha takribani asilimia 10 ya hisa za familia, jambo lililochangia ongezeko la utajiri wa familia ya Trump kupitia sekta ya sarafu za kidijitali.