Iddi Kajuna wa Simba Sports Club Afariki Dunia

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 hour ago
rickmedia: iddi-kajuna-simba-sports-club-afariki-dunia-127-rickmedia

Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu ya Simba, Iddi Kajuna amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Julai 23, 2026 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa mujibu wa taarifa ya leo Julai 23, 2026 iliyotolewa na uongozi wa Simba SC, mwili wa marehemu Kajuna utaswaliwa katika Msikiti wa Maamur Upanga na utazikwa katika Makaburi ya Kisutu Dar es Salaam leo Saa 10 Alasiri.

Kajuna aliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo mwaka jana na amehudumu kwenye nafasi hiyo hadi mauti yanamkuta huku kazi yake ya mwisho ikiwa ni Fainali ya Kombe la CRDB iliyofanyika Visiwani Pemba Julai 4 mwaka huu ambapo pia alikua Mjumbe wa Baraza la ushauri lilioundwa na Rais wa klabu hiyo Mohammed Dewji.

Kabla ya hapo Kajuna amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba mwaka 2017 na Mjumbe wa kamati ya utendaji kuanzia mwaka 2014-2018 huku akiwahi kuwa Mjumbe wa Bodi ya mpito ya Wakurugenzi mwaka 2018 wakati wa mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa Uongozi.