Mwanamitindo na nyota wa vipindi vya televisheni, Kylie Jenner, amefanya mzaha kuwa anafikiria kuongeza zaidi ukubwa wa maziwa yake baada ya kufanya upasuaji wa plastiki (cosmetic surgery) hapo awali.

Akiwa kwenye mazungumzo katika kipindi cha podcast cha Better Half with Stas & Vic, kilichoendeshwa na marafiki zake wa karibu Stassie Karanikolaou na Victoria Villarroel, Kylie aligusia uamuzi wake wa zamani wa kuweka wazi maelezo kuhusu upasuaji huo.
Mwanadada huyo, ambaye huko nyuma aliwahi kuweka wazi kuwa saizi ya viwekeo vyake vya maziwa (breast implants) ni 445cc, alitania kuwa saizi hiyo kwa sasa haimtoshelezi tena.
"Nataka maziwa yangu yawe yanaingia chumbani kabla yangu," alitania Kylie, akidokeza uwezekano wa kuchagua saizi kubwa zaidi siku zijazo.
Marafiki zake walithibitisha kuwa nia hiyo si ngeni kwani Jenner amekuwa akizungumzia hamu yake ya kuongeza saizi hiyo kwa takribani mwaka mmoja sasa. Uamuzi huo unaonyesha jinsi nyota huyo anavyoendelea kuwa wazi kuhusu muonekano wake na mabadiliko ya mwili wake.