Mwalimu wa zamani wa Shule ya Sekondari Angleton nchini Marekani, Holly Adams, amekamatwa na jeshi la polisi kufuatia tuhuma za kuwa na uhusiano usiofaa wa kimapenzi na wanafunzi wake.
Adams anakabiliwa na mashtaka ya kuharibu ushahidi pamoja na kuwauzia au kuwapa pombe watoto wadogo. Uchunguzi uliochukua pindi cha mwaka mzima ulianza baada ya mwanafunzi kutoa taarifa kuwa alimwona mwalimu huyo kwenye simu ya video (FaceTime) akiwa chumbani na mwanafunzi wa zamani, pamoja na kuwepo kwa picha za utupu. Pia, anatuhumiwa kuwakaribisha wanafunzi nyumbani kwake na kuwasiliana na wachezaji wa timu ya shule kupitia mtandao wa Snapchat.
Mwalimu huyo ameshafutwa kazi na shule hiyo, na hivi sasa yupo nje kwa dhamana ya dola 26,000 huku uchunguzi zaidi ukiendelea.