Madaktari nchini Sri Lanka wamefanikiwa kuondoa jiwe lenye uzito wa kilo 3.1 kwenye kibofu cha mkojo cha mwanaume mwenye umri wa miaka 55.
Upasuaji huo ulifanyika katika Hospitali Kuu ya Trincomalee, baada ya mwanaume huyo kulazwa akilalamikia maumivu makali. Jiwe hilo lenye urefu wa sentimita 17 linaaminika kuwa moja ya mawe makubwa kuwahi kuondolewa katika kibofu cha mkojo.