Rais wa Slovenia, Nataša Pirc Musar apigwa faini kwa kutokufunga mkanda wa gari

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

14 hours ago
rickmedia: rais-slovenia-natasa-pirc-musar-apigwa-faini-kwa-kutokufunga-mkanda-gari-390-rickmedia

Rais wa Slovenia, Nataša Pirc Musar, amepigwa faini ya euro 120 baada ya kubainika kuwa hakuwa amefunga mkanda wa usalama wakati gari lake lilipohusika katika ajali.

Ajali hiyo ilimuacha Rais Pirc Musar akiwa na jeraha la kuvunjika mfupa wa bega. Wakati huo huo, dereva wake anaendelea kuchunguzwa kutokana na tuhuma za kutofuata baadhi ya taratibu za usalama barabarani.

Akizungumzia tukio hilo, Rais huyo aliomba radhi kwa wananchi na kukiri kuwa kutofunga mkanda wa usalama ilikuwa ni “kosa kubwa”.