Aliyekuwa mke wa Mhasibu wa Diamond Platnumz 'Juju' amethibitisha kuachana na mume wake Don Fumbwe kwa kile alichokiita kuchagua amani ya moyo wake na watoto wake.
Juju amepost picha yake pamoja na @donfumbwe na kuiweka alama ya 'X' na kuweka ujumbe unaoashilia hawako pamoja huku akisisitiza kuwa "Mimi sio mke wa mtu tena".


Juju ameelezea kuwa mume wake ana mtu mwingine (Mahusiano mengine) na alipomwambia achague kati ya hayo mahusiano mapya na familia yake (Yeye mke wake na watoto wao wawili) Fumbwe alimchagua mwanamke wake mpya na kuiacha familia yake.