Trey Songz amshtaki Promota, ataka alipwe Bilioni 1.3

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 hour ago
rickmedia: trey-songz-amshtaki-promota-ataka-alipwe-bilioni-13-157-rickmedia

Msanii Trey Songz amefungua kesi dhidi ya promota wa tamasha huko Texas, akidai kuwa promota huyo hakutimiza makubaliano yao kuhusu show aliyokuwa amepangiwa kufanya.

Kwa mujibu wa kesi hiyo, kampuni ya Trey Songz ilifanya makubaliano na promota Darryl Austin mwezi Aprili, ambapo Trey alitakiwa kufanya tamasha katika Ukumbi Wa Will Rogers Auditorium, Fort Worth, Texas, tarehe 8 Agosti, 2026.

Hata hivyo, Trey anadai kuwa promota huyo hakutimiza wajibu wake kama walivyokubaliana, jambo lililosababisha hasara kwake na kwa kampuni yake. Sasa Trey amefungua kesi mahakamani akidai zaidi ya dola 500,000 (Tsh. Bilioni 1.3/=) kama fidia.