Producer Dr.Dre aipokei AI kwenye mambo yake ya Production

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: producer-drdre-aipokei-kwenye-mambo-yake-production-732-rickmedia

Dr. Dre ametoa maoni yake kuhusu nafasi inayozidi kukua ya teknolojia ya Akili Mnemba (AI) katika muziki.

Katika mahojiano na The New York Times akiwa pamoja na mshirika wake wa muda mrefu wa biashara Jimmy Iovine, rapa na producer huyo maarufu alisema AI ni “zana mpya ya ubunifu” na kwamba haioni teknolojia hiyo kama “tishio.”

Katika mahojiano hayo yaliyochapishwa Jumapili, Agosti 23, Dre alilinganisha upinzani unaoonekana sasa dhidi ya AI na mashaka yaliyokuwepo zamani wakati drum machines na synthesizers zilipoanza kuingia katika utengenezaji wa muziki.

“Nilikuwa na mazungumzo na watu kadhaa siku chache zilizopita,” Dre aliiambia Times. “Walikuwa wanapinga AI, nikawaambia, ‘Sawa, mnasikika kama watu ambao wangepinga drum machine ilipotokea.’ Au synthesizers, sio? Hii ni zana mpya ya ubunifu. Baadhi ya watu wanaogopa kujifunza vitu vipya.”

Dre pia alikiri kuwa tayari anatumia AI katika muziki wake mwenyewe, akieleza kwamba anaichukulia teknolojia hiyo kama zana ya kujaribu kuona inaweza kufanya nini na kile ambacho yeye tayari ametengeneza.

“Nimeikubali. Nasubiri kwa hamu kuona nini kitatokea kupitia teknolojia hii,” aliongeza.

Staa huyo wa zamani wa kundi la N.W.A pia alipinga hoja kwamba AI yenyewe ni tishio kwa wanamuziki.

“Nadhani watu pekee wanaoiona kama tishio ni wale ambao wana matatizo katika kutengeneza vitu vipya,” alisema producer huyo.

Jimmy Iovine naye alionesha mtazamo chanya kuhusu matumizi ya AI katika muziki.

Mkongwe huyo wa tasnia ya muziki alisema kuna “AI producers wengi wanaoitumia kwa siri,” kauli ambayo Dre aliikubali na kusema: “Hiyo ni njia nzuri ya kuiweka. Wanaitumia, ila hawataki kukiri.”

Iovine alisema anaunga mkono sana matumizi ya AI katika utengenezaji wa muziki na haoni hasara kubwa inayoweza kutokana nayo.

“Kutakuwa na muziki mbaya. Muziki mbaya upo hata sasa. Lakini watu wenye vipaji wanapokuwa studio na kuwa na AI, watatengeneza rekodi bora zaidi,” alisema.

Dre na Iovine walishirikiana kuanzisha Beats Electronics na Beats Music kabla ya kuiuza Beats kwa Apple mwaka 2014 katika dili lililoripotiwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola bilioni 3.