Duane "Keffe D" Davis akutwa na hatia kifo cha Rapa Tupac

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 hour ago
rickmedia: duane-keffe-davis-akutwa-hatia-kifo-cha-rapa-tupac-898-rickmedia

Duane "Keffe D" Davis, aliyekuwa mwanachama wa genge la mjini Los Angeles, Marekani amepatikana na hatia ya kumuua rapa maarufu Tupac Shakur mwaka 1996.

Baada ya takriban miaka 30 tangu kifo cha Tupac, mahakama ya Las Vegas ilimhukumu Davis, mwenye umri wa miaka 63, kwa kosa la mauaji ya daraja la kwanza kwa kutumia silaha ya moto.

Davis, ambaye anakabiliwa na kifungo cha maisha jela bila msamaha, amesema atakata rufaa kupinga hukumu hiyo.