Ndege ya mizigo yaua watu wapatao watano (5) Miami Nchini Marekani

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: ndege-mizigo-yaua-watu-wapatao-watano-5-miami-nchini-marekani-511-rickmedia

Watu wasiopungua watano wamethibitishwa kupoteza maisha baada ya ndege ya mizigo ya kampuni ya Amazon Prime Air kupata ajali mbaya wakati ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami siku ya Jumapili.

Ndege hiyo, iliyokuwa kwenye Safari Nambari 7598, ilishindwa kusimama na kupitiliza njia yake ya kutua (runway) mnamo saa 8:00 mchana.

Viongozi wa eneo hilo wameeleza kuwa, baada ya kupitiliza uwanjani hapo, ndege hiyo ilienda kugonga magari kadhaa yaliyokuwa katika eneo hilo, jambo lililopelekea vifo vya watu hao watano au zaidi.

Uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo bado unaendelea.