Trump apendekeza jina jipya la Akili Bandia (AI)

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 hour ago
rickmedia: trump-apendekeza-jina-jipya-akili-bandia-ai-822-rickmedia

Rais wa Marekani Donald Trump amependekeza jina jipya la teknolojia ya akili bandia (AI) akiiita Super Intelligence (SI).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka BBC News akizungumza katika hotuba yake, Trump amesema matumizi ya neno “artificial”, linalomaanisha bandia, yanaweza kufanya teknolojia hiyo ionekane kama siyo kitu halisi.

Amesema, “Kutumia neno ‘bandia’ kunafanya ionekane kama kitu ambacho siyo halisi. Siyo hivyo, kwa kweli ni jambo la kushangaza. Lakini tunapaswa kuwa waangalifu.”

Trump pia amesema, “Karibuni katika ulimwengu mpya wa akili iliyoboreshwa.”

Hapo awali, Trump amesema nchi itakayoshinda katika mashindano ya AI itakuwa mshindi, huku akipinga kuwekwa kanuni kali za kudhibiti teknolojia hiyo.

Msimamo huo wa Trump unatofautiana na baadhi ya viongozi.