Tyson adai Diddy alimuomba amfikishie barua yake kwa Rais Trump

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 hour ago
rickmedia: tyson-adai-diddy-alimuomba-amfikishie-barua-yake-kwa-rais-trump-80-rickmedia

Bondia Mike Tyson kwenye interview na 'Billboard Hiphop' ameweka wazi kuwa Sean “Diddy” Combs alimwomba amfikishie Rais Donald Trump barua kwa niaba yake.

Tyson alipoulizwa kama aliifikisha barua hiyo kwa rais, alijibu kuwa alifanya kile ambacho Diddy alimwomba afanye.

Barua hiyo ilikuwa na lengo la kumwomba Trump amsamehe Diddy kupitia mamlaka ya rais ya kutoa msamaha (presidential pardon), hatua ambayo inaweza kumuondolea au kumpunguzia adhabu ya kisheria, kulingana na aina ya kesi.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa Diddy kujaribu kuwasiliana na Trump kuhusu suala hilo. Awali, Trump aliwahi kusema kuwa Diddy alikuwa amemtumia barua nyingine iliyoandikwa kwa mkono, akiomba msamaha.

Diddy Amehukumiwa Kifungo Cha Miaka Minne (4) Jela Kwa Kesi Za Kingono, Na Anatarajia Kuachiwa Huru March 2028.