Mchungaji ahukumiwa miaka 12 Jela kwa kumbaka muumini na kumrekodi Video

-rickmedia: Rick

Rick

18 hours ago
rickmedia: mchungaji-ahukumiwa-miaka-jela-kwa-kumbaka-muumini-kumrekodi-video-616-rickmedia

Mchungaji mmoja wa Kinigeria anayeishi nchini Uingereza, Brein Ayeni (43), amehukumiwa kifungo cha miaka 11 na miezi tisa jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka muumini wake mara kwa mara na kumfanyia vitendo vya unyanyasaji wa kisaikolojia.

Ayeni, ambaye alikuwa kiongozi wa kanisa la Christworld Nation Church huko Coventry, alikuwa akirekodi baadhi ya matukio hayo kwenye simu yake. Baada ya hapo, alitumia video hizo kumtishia mwanamke huyo asithubutu kwenda polisi, akimwambia akitoa taarifa tu atazisambaza na kudai walikuwa na makubaliano.

Zaidi ya hapo, alikuwa akimdhalilisha kwa maneno kuhusu maisha yake ya nyuma ili kumvunja nguvu.

Ukatili huo ulianza tangu Juni 2025, lakini mwanamke huyo alijikusanya na kwenda kutoa taarifa polisi Machi 2026. Baada ya kesi kusikilizwa katika Mahakama ya Warwick Crown, mchungaji huyo alikutwa na hatia ya makosa matatu ya ubakaji na kosa moja la kumnyanyasa na kumdhibiti mwathiriwa, na Novemba 10, 2026 mahakama ikamhukumu kwenda jela.