Zombie @s2kizzy ameipa nyota 5 ngoma ya @rayvanny feat @diamondplanumz "TETEMA" kuwa ndio Wimbo mkubwa zaidi kuwahi kufanyika Tanzania.
S2kizzy ameandika hayo kupitia Instastory yake. Pamoja na kuwa ngoma nyingi kubwa za kizazi hiki zimepita mikononi mwake lakini S2kizzy ameichagua TETEMA ambayo pia ameipika yeye mwenyewe.