Baada ya miaka 15 ya kuibeba jezi ya Colombia, James Rodríguez ametangaza kustaafu soka la kimataifa akiwa na miaka 35. Kutoka kwenye usiku wa kihistoria wa Brazil 2014, aliposhinda Golden Boot kwa kufunga mabao 6, hadi kuwa nahodha na mmoja wa wachezaji muhimu zaidi katika historia ya La Tricolor.
James anaondoka akiwa amecheza mechi 131, akifunga mabao 31 na kutoa assists 43 kwa Colombia. Pia aliongoza Colombia hadi fainali ya Copa América 2024, ambako alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo.
Kutoka Monaco hadi Real Madrid, Bayern Munich na klabu nyingine mbalimbali, James ameacha alama kubwa kwenye soka la dunia.
Kipaji, pasi za kisanii, free-kicks na ile left foot yake vitabaki kuwa sehemu ya fikra zetu