Papa aina ya 'Nurse Shark* mwenye rangi ya machungwa 'Orange' inayong'aa vizuri kabisa aligunduliwa karibu na Hifadhi ya Taifa ya Tortuguero nchini Costa Rica mwaka 2024.
Watafiti walihusisha rangi yake na macho yake meupe na mchanganyiko adimu sana wa hali ya 'Xanthism' na 'Albinism' tukio la kwanza kabisa kurekodiwa kwa aina hiyo ya papa.
Licha ya kupoteza uwezo wake wa asili wa kujificha (kwa kuendana na mazingira), papa huyo mwenye urefu wa futi sita alifanikiwa kuishi hadi kufikia utu uzima.