Mwanamuziki wa nyimbo za asili Saida Karoli amefunguka kuwa kuna nyakati alipitia mambo magumu ambayo hawezi kuyasema kwa watu.
Saida ameiambia Clouds Tv kuwa "Nilipatwa na majanga makubwa, wapo waliozusha nimekufa, nimezeeka sana siwezi hata kutembea. Na pia nilipishana kauli na manager wangu. Nilizichukia sana nyimbo zangu za zamani. Na wale madansa wangu wa nyimbo za Kaisiki na nyinginezo walio wengi walifariki. Zile nyimbo nilizichukia sana na nilipokuwa nikiwaona kwenye video wale madansa wangu waliofariki nilikuwa nalia sana."
"Nilitamani kuacha kuimba. Nilianza kumtafuta Ruge Mutahaba naye akawa amefariki na yaliyonikumba ni mengi. Pia nilifiwa na mwanaume wangu aliyekuwa ananisaidia alidumbukia kwenye kisima cha maji na kufariki dunia aliniacha na ujauzito. Nilipatwa na mikasa mingi ambayo haifai kuwasimulia Watanzania. Nilijikuta narudi nyuma sana. Kwa sasa najihisi faraja sana"