Aliyekuwa nyota wa soka wa Brazil, Dani Alves, na mkewe mwanamitindo wa Kihispania, Joana Sanz (34), wameripotiwa kuwa katika mchakato wa kuachana (talaka) baada ya ndoa ya miaka tisa, ikielezwa kuwa sababu kuu ni mwanasoka huyo kujikita zaidi katika shughuli za kuhubiri Injili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya Ijumaa Novemba 13, Sanz alithibitisha kuwa wametengana kwa muda sasa baada ya shabiki kumuuliza iwapo huambatana na mumewe kwenye ibada.
"Mimi siyo muumini hata kidogo. Kadiri ninavyoona anachokifanya, ndivyo ninavyozidi kujitenga na mambo hayo. Napenda pia kuweka wazi kuwa tumetengana kwa muda sasa, kwa sababu hiyo hiyo," aliandika Sanz.