Rapa Nicki Minaj anakabiliwa na madai kutoka kampuni yake ya zamani ya mawakili, Gordon Rees Scully Mansukhani, ambayo inadai hajalipa ada za uwakili.
Kampuni hiyo inasema Nicki anadaiwa jumla ya $295,605 kutokana na huduma za kisheria katika kesi ya Hakimiliki (copyright) kuhusu wimbo wake “I Lied.”
Kesi hiyo ilimalizika kwa makubaliano ya siri mwishoni mwa mwaka 2024. Sasa Kampuni hiyo imeiomba mahakama kutoa hukumu ya upande mmoja (default judgment), ambayo inaweza kumlazimisha Nicki kulipa kiasi hicho iwapo mahakama itakubaliana na madai yao.
Hata hivyo, madai hayo bado ni madai ya kampuni ya mawakili, na si uthibitisho wa mwisho kwamba Nicki ana deni hilo.