Mahakama nchini Saudi Arabia imemhukumu mfanyakazi wa ndani raia wa Kenya, Esther Wanja Muthoni (40), bakora 100 na kifungo cha mwaka mmoja cha kutojihusisha na jamii (marufuku) baada ya kupatikana na hatia ya kupata ujauzito na kujifungua nje ya ndoa.
Muthoni alipata ujauzito baada ya kuwa kwenye uhusiano wa muda mfupi na mwanamume raia wa Misri ambaye baadaye aliondoka nchini humo. Baada ya kujifungua Agosti 2025, alikamatwa na polisi na kufunguliwa mashitaka.
Akiwa hana wakili, Muthoni aliamua kutokata rufaa dhidi ya hukumu hiyo ili kuepuka kuchelewesha safari yake ya kurejea nyumbani Nairobi kwa wanaye watano.