Joeboy Aleta Burudani ya Sikukuu Afrika Mashariki Kupitia Wimbo Mpya “Pretty Girls”

-rickmedia: Rick

Rick

8 hours ago
rickmedia: joeboy-aleta-burudani-sikukuu-afrika-mashariki-kupitia-wimbo-mpya-pretty-girls-891-rickmedia

Msanii nyota wa Afropop kutoka Nigeria, Joeboy, analeta wimbo wake mpya unaoitwa “Pretty Girls” kwa mashabiki wa Afrika Mashariki. Wimbo huo tayari unapatikana kwenye majukwaa yote makubwa ya kusikiliza muziki mtandaoni, huku video yake rasmi ikipatikana YouTube.

“Pretty Girls” ni wimbo wenye midundo ya uchangamfu na furaha unaosifia wanawake, kujiamini kwao, mitindo yao ya mavazi na nguvu wanayoleta wanapokuwa kwenye uwanja wa dansi. Ukiwa umetayarishwa na Kevin Chukwunenye Akpevwe, wimbo huu unaunganisha midundo ya gitaa yenye mvuto na mapigo ya muziki yanayochangamsha, huku Joeboy akitumia sauti yake laini na yenye melodi nzuri.

Tofauti na nyimbo zake za hivi karibuni zilizogusia maumivu ya mapenzi, safari hii Joeboy anawaletea mashabiki muziki wa furaha, burudani na kuthamini uzuri wa wanawake.

Video ya wimbo huo inaendana kikamilifu na ujumbe wake. Ikiwa imerekodiwa katika mazingira ya sherehe za wikendi yenye mwanga wa jua, video hiyo inaonesha mitindo ya mavazi yenye mvuto, mandhari yenye rangi mbalimbali na madansi yenye nguvu, huku Joeboy akiwa kitovu cha burudani hiyo.

Wimbo “Pretty Girls” pia unatoa hamasa kuelekea mradi wake mpya wa muziki unaoitwa Lavida Boy EP, wenye jumla ya nyimbo tano, utakaotoka rasmi Novemba 20, 2026.


Afrika Mashariki Kujiandaa kwa Msimu wa Sherehe

Kwa muda mrefu, Afrika Mashariki imekuwa moja ya maeneo yanayoupenda muziki wa Joeboy. Wimbo wake wa mwaka 2019, “Beginning”, uliingia kwenye orodha ya nyimbo 10 bora za Apple Music nchini Kenya na Uganda.

Kupitia “Pretty Girls”, Joeboy anarejea katika eneo hili wakati ambapo msimu wa sherehe za mwisho wa mwaka unakaribia kuanza. Katika wiki zijazo, mashabiki wa Nairobi, Kampala na Dar es Salaam watapata fursa ya kushiriki changamoto ya dansi ya #PrettyGirlsNoStress kupitia TikTok na Instagram.

Ushiriki ni rahisi: Kusanya marafiki zako, cheza kwa kutumia sehemu ya wimbo huo inayovutia zaidi, kisha watag marafiki zako wa kike. Video bora za makundi katika kila soko zitajishindia nafasi za VIP katika matukio maalumu ya “Pretty Girls” yatakayofanyika mwezi Desemba.


Tazama na Sikiliza

* Video Rasmi: YouTube

* Sikiliza Wimbo: Spotify na Apple Music

* Jiandae kwa EP ya Lavida Boy: Pre-save


Kuhusu Joeboy

Joeboy, anayejulikana kwa jina lake halisi Joseph Akinfenwa-Donus, ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Nigeria anayejulikana kwa muziki wake wa Afropop wenye melodi nzuri na nyimbo zinazogusia mapenzi.

Aligunduliwa na msanii Mr Eazi mwaka 2016 kupitia video aliyoweka Instagram akiimba wimbo wa Ed Sheeran uitwao “Shape of You”. Umaarufu wake ulianza kupaa zaidi kupitia wimbo wake “Baby” mwaka 2019. Baadaye alitoa nyimbo zilizopata mafanikio makubwa zikiwemo “Beginning” na “Sip (Alcohol)”.

Pia alishirikiana na Mr Eazi kwenye wimbo “Nobody” wa DJ Neptune, ambao ulikuwa miongoni mwa nyimbo kubwa za Afrika mwaka 2020.

Joeboy ameshatoa albamu mbili, Somewhere Between Beauty & Magic (2021) na Body & Soul (2023). Mwaka 2024 alianzisha lebo yake binafsi ya muziki iitwayo Young Legend.