Baada ya kuwepo na Taarifa za kuwa Msanii Mbosso Ameondoka Katika lebo ya WCB, CEO wa Lebo hiyo Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza Ametoa kauli kuhusu stori za Msanii Mbosso kuondoka ndani ya Lebo hiyo.
Kupitia Insta story ya #Diamond amesema kuwa wamekuwa na mazungumzo mazuri na #Mbosso namna ya kuanza rasmi kusimamia Kazi zake.
Mbali na hivyo #Diamond amesema kuwa Stori yoyote inayomuhusu #Mbosso ipuuzwe Mpaka mwenyewe atoe Tamko.
Taarifa za Mbosso Kuondoka WCB zilianzishwa na mtu wa karibu na Diamond Platnumz na Mtangazaji wa Wasafi FM Baba Levo ambe alisema kuwa Mbosso ni rasmi ameondoka kwenye lebo hiyo na hajalipishwa kiasi chochote cha Pesa kama wasanii wengine walivyoondoka akiwazungumzia Harmonize na Rayvanny ambao walilipia kiasi cha Pesa.
Baada ya kauli ya Diamond Platnumz, Baba Levo ameibuka tena na kukana kauli zake kuhusu Mbosso kuondoka WCB na kusema kuwa zipuuzwe na isubiriwe kauli ya CEO ambae ni Diamond.