Kanye West na Mkewe wazua gumzo kwenye Red Carpet ya Tuzo za Grammy

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: kanye-west-mkewe-wazua-gumzo-kwenye-red-carpet-tuzo-grammy-151-rickmedia

Msanii wa Marekani, Kanye West na mkewe, Bianca Censori, waliwaacha watu midomo wazi katika usiku wa tuzo za Grammy zilizofanyika katika Ukumbi wa Crypto.com jijini Los Angeles usiku wa Februari 2, 2025.

Kanye West aliwasili akiwa amevalia mavazi meusi juu mpaka chini huku mkewe Censori aliyekuwa ameambatana naye ambaye mwanzoni alivaa koti kubwa la manyoya lakini walipokuwa wanatembea kwenye zulia jekundu, Censori alilivua koti hilo na sehemu za mwili wake kuonekana wazi kutokana na gauni jepesi alilokuwa amevaa.

Muda mfupi baada ya kuwasili wawili hao pamoja na wapambe wao, waliombwa kuondoka mahali hapo huku ripoti zikidai kuwa wanandoa hao hawakualikwa rasmi kwenye hafla hiyo.

Kanye West aliteuliwa kuwania kipengele cha Best Rap Performance kwa wimbo wake "Carnival," lakini tuzo hiyo ilikwenda kwa Kendrick Lamar.

Hata hivyo, kitendo alichofanya Censori kimeibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii huku wengine wakisema kuwa mwanadada huyo ni mbunifu aliyeelimika na huwa anafanya maamuzi ya kimakusudi ili kuvutia watu.