Msanii Selena Gomez alijikuta akilia kutokana na sera za uhamiaji za Donald Trump na jinsi zinavyoathiri watu wake. Kupitia ukurasa wa Instagram wa Staa wa Muziki #SelenaGomez alishare video akimwaga machozi kisa tishio la Rais wa Marekani #DonaldTrump la kuwafukuza wahamiaji kwa wingi, ambalo limeibua hofu ya kutenganishwa kwa familia za wengi.
Staa huyo mwenye miaka 32 aliyezaliwa Texas Familia yake ilihamia Marekani Mwaka 1970 wakitokea Mexico.