Mwanamke mmoja ameitisha ulinzi wa kisheria dhidi ya mume wake, akimtuhumu kwa kutishia kuchoma moto nyumba yao kila anapokataa matakwa yake ya ndoa, hata wakati wa hedhi yake.
Mwanamke huyo kutoka Zimbabwe, #GraterNyambizi, aliieleza mahakama kuwa anaishi kwa hofu kila wakati kwa sababu ya mume wake, #TrustChinyanga, ambaye anaamini anaweza kutekeleza vitisho vyake kwa hasira.
Pia alidai kuwa #Chinyanga humshutumu mara kwa mara kwa uzinzi na humshambulia kwa matofali kila anapochelewa kurudi nyumbani kutoka kazini.
Katika utetezi wake, Chinyanga alikiri kuwa masuala ya ndoa yalikuwa chanzo cha migogoro yao, lakini akasema tatizo halisi ni mtazamo wa Nyambizi juu yake.
Hakimu Meenal Naratom alieleza wasiwasi wake juu ya tabia ya Chinyanga, hasa kuhusu kulazimisha tendo la ndoa wakati mke wake anapojisikia kutokuwa tayari.
"Kwa nini unamlazimisha mke wako kushiriki tendo la ndoa ikiwa hajisikii vizuri?" aliuliza hakimu.
Katika uamuzi wake, Hakimu Naratom alitoa amri ya ulinzi kwa Nyambizi na akashauri wanandoa hao kutafuta ushauri wa ndoa.