Mtangazaji wa zamani wa CNN #DonLemon amekanusha madai ya rapa #KanyeWest kumshutumu kwa kuripoti uongo kwamba yeye na mkewe, Bianca Censori, walifukuzwa kwenye Tuzo za #Grammy.
"Huyu ndiye mjinga aliyeanzisha uvumi kwamba mimi na mke wangu tulifukuzwa kwenye Grammys. Miongo mitatu ya kuleta ubunifu katika muziki na bado kuna *** kama huyu,” West aliandika kwenye chapisho la Instagram ambalo sasa limefutwa, pamoja na picha ya Lemon.
Licha ya kuwashangaza wengi kwenye Red Carpet ya Tuzo za #Grammy #Ye na Mke wake #BiancaCensori na kusemekana hawakuingia kwenye ukumbi Tuzo hizo zilipokuwa zikifanyika kutokana na kufukuzwa kwa Mujibu wa #ET.
#TMZ imekanusha taarifa hizo na kusema kuwa Mmoja ya wahusika wa Tuzo za #Grammy amesema kuwa #KanyeWest alikuwa ni Mmoja ya Wageni Walikuwa kwenye List na alikuwa anawania katika Kipengele cha #BestRapSongOfTheYear .
Pia aliongeza kwa kusema kuwa taarifa za #Ye na Mke wake kuondoka baada ya kutoka kwenye Red Carpet na kwenda kwenye Gari Yao iyo ni mambo Yao wenyewe hakuna hakuna mtu wa #Grammy Wala polisi waliowafukuza.