Rais wa Marekani #DonaldTrump anapanga kuhudhuria #SuperBowl huko New Orleans Jumapili, ikiwa ni mara ya kwanza kwa rais aliye madarakani kuhudhuria mchezo huo.
Mechi ya Super Bowl 59 kati ya Kansas City Chiefs na Philadelphia Eagles inafanyika mwezi mmoja baada ya mshambuliaji wa kigaidi kuendesha lori kwenye Mtaa wa Bourbon huko New Orleans siku ya Mwaka Mpya, na kusababisha vifo vya watu 14 na kuwajeruhi wengine wengi.
Maafisa walisema Jumatatu kwamba hakuna vitisho vya kuaminika kwa mchezo huo au matukio yake mengi yanayoambatana nayo.