Mkurugenzi wa lebo ya WCB Wasafi Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ametangaza kuongeza msanii mwingine kwenye lebo yake kwa ku-share mkataba wake.
Diamond Platnumz amempost mwanasheria wake akiwa na mkataba na kuandika ni kiasi gani ana furaha ya kufanikisha hilo.
Msanii huyo aliyesainiwa hajawekwa wazi kwa jina wala sura, ikumbukwe msanii huyo amesainiwa ikiwa ni wiki kadhaa tangu iwekwe wazi kuwa Mbosso hayupo tena kwenye lebo hiyo.
Usajili wa msanii huyo kwenye lebo hiyo unaufuata usajili wa msanii D-Voice aliyesainiwa WCB Wasafi Mwaka 2023 na kutangazwa rasmi usiku wa Novemba 17, 2023 ikiwa sambamba na kuitambulisha Album yake ya kwanza akiwa chini ya WCB aliyoipa jina la (Swahili Kid)