Shura Ya Maimamu: Bunge lifute sheria kandamizi zilizotajwa na Tume ya Jaji Nyalali

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: shura-maimamu-bunge-lifute-sheria-kandamizi-zilizotajwa-tume-jaji-nyalali-604-rickmedia

Shura ya Maimamu Tanzania imetoa wito kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lizifute Sheria zote kandamizi katika Mfumo wa Sheria wa Taifa, ikiwemo zilizotajwa na Tume ya Jaji Nyalali (1991).

Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu, Sheikh Ponda Issa Ponda amesema “Sheria nyingine kandamizi ya kufutwa ni ile inayoitwa ya kupambana na Ugaidi. Inamnyang’anya mtuhumiwa Haki zake zote za msingi, inatumika kuwatuhumu na kuwakamata Watu wa Imani hasa Waislamu. Kiasi kwamba imejengwa dhana kwa Wananchi kuwa Serikali ya Tanzania ina ajenda dhidi ya Uislamu na Waislamu.”

Amesema hayo kupitia Waraka wa Eid Al-Fitr, Machi 31, 2025, akiongeza “Pia, tunaikumbusha Serikali ipeleke ushahidi Mahakamani ili Waislamu wakiwemo Masheikh, Maimamu, Waalimu wa Madrasa, Wasomi wa Vyuo Vikuu na Waumini wa kawaida, inaowashikilia kwa tuhuma za ugaidi wapate Haki yao ya kujitetea na kusomewa hukumu.”