Kanye West na Kim Kardashian wameingia kwenye mvutano mkali baada ya Kanye West kuachia wimbo wake mpya "Lonely Roads Still Go to Sunshine," unaodaiwa kumshirikisha binti yao, North West, pamoja na Diddy na Christian Combs. Kim alijaribu kutumia mahakama kuzuia wimbo huo, akisema hakutaka North kushiriki.
Kwenye chati azlizoweka kwenye X, Kanye alimshutumu Kim kwa kusajili jina la North kama alama ya biashara bila ridhaa yake, lakini Kim alidai alimuuliza na Kanye alikubali. Alisisitiza kuwa alimtumia nyaraka kuhakikisha North hashiriki kwenye wimbo Na Diddy kwa usalama wake. Kanye alijibu kwa ukali, akitishia "vita vya hadhara" iwapo hakutakuwa na mabadiliko.
Kim alijaribu kumzuia kisheria Kanye kuachia wimbo huo, lakini Kanye hakuhudhuria kikao cha upatanishi. Wimbo huo ulirekodiwa baada ya North kutembelea studio ya baba yake kwa mara ya kwanza baada ya wiki kadhaa bila kumuona.
Kim anataka kumlinda North dhidi ya mgogoro wa Kanye na Diddy, hasa kutokana na matatizo ya kisheria yanayomkabili Diddy. Wakati huohuo, Kanye ameonyesha kumuunga mkono Diddy hadharani, akishutumu watu maarufu kwa kutomsaidia.